Romans 12:8-13

8 akama ni kutia moyo na atie moyo, kama ni kuchangia kwa ajili ya mahitaji ya wengine na atoe kwa ukarimu, kama ni uongozi na aongoze kwa bidii, kama ni kuhurumia wengine na afanye hivyo kwa furaha.

Alama Za Mkristo Wa Kweli

9 bUpendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema. 10 cPendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine. 11 dMsiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana. 12 eKuweni na furaha katika tumaini, katika dhiki kuweni na saburi, dumuni katika maombi. 13 fChangieni katika mahitaji ya watakatifu, wakaribisheni wageni.

Copyright information for SwhKC